Social Icons

Sunday 13 October 2013

MBEYA CITY: LAZIMA TUSHIKE USUKANI.


MBEYA City imechupa hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara na kocha mkuu wa timu hiyo, Juma Mwambusi amesema lazima wahakikishe wanaonja usukani wa ligi ili kuweka heshima.

Mbeya City, timu mpya kwenye ligi msimu huu ina pointi 14 sawa na Azam iliyo nafasi ya pili lakini wanatofautiana mabao ya kufunga na kufungwa huku wakiwa nyuma kwa pointi moja kwa vinara wa ligi, Simba.

Mwambusi alisema: “Hayo maneno wanayoongea kutuponda kuwa tumeanza ligi kwa nguvu ya soda, sijui tumetoa sare nyingi hatufiki mbali, hayo ni maneno tu na wivu, tena wengine ni makocha maarufu nashangaa kwa nini wanathubutu kusema maneno kama hayo ila sisi tunasonga mbele mpaka washangae.”

“Kukaa kileleni inawezekana, hii ni ligi na haina mwenyewe, Simba yuko juu na anaweza kushuka na kukaa mwingine yeyote ikiwamo sisi na nitafurrahi malengo yetu ya kuhakikisha tunakamata usukani wa ligi yakitimia msimu huu hata kwa mara moja,” alisema Mwambusi.

Chanzo:- Mwanaspot.

1 comment:

Mpaju said...

HONGERA MBEYA CITY. Lakini usia wangu kwa MWAMBUSI,ni huu. Kwa sasa mtazamo uwe kwenye mfumo wa KUCHUMI zaidi ya malumbano ya SOKA na hawa walioshindwa kulipeleka soka letu popote miaka na miaka. UWANJA wetu, wanachama HAI, vitegauchumi na kadhalika ndio vitu ambavyo vinahitajika MAKOMBE yatafuata tena mengi sana.

 
 
Blogger Templates