Social Icons

Monday, 10 March 2014

MGOMBEA WA CCM JIMBO LA KALENGA GODFREY MGIMWA AFANYA KAMPENI NA MVUA KUBWA

 Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Ndugu Godfrey Mgimwa akiwa amebebwa juu na mmoja wa wanakijiji,mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa kampeni wa uchaguzi mdogo wa jimbo hilo,uliofanyika katika kijiji cha Wenda kata ya Mseke-Iringa Vijijini,huku kukiwa na mvua kubwa ikinyesha,ambayo hata hivyo haikuzuia kufanyika kwa mkutano huo.Wananchi wa Kijiji hicho walionekana kuw ana shauku kubwa ya kutaka kumsikiliza Mgombea huyo bila kujali kulowana na mvua.Uchaguzi unatarajiwa kufanyika Machi 16.
 Wanakijiji cha Wenda wakimpungia Mgombea Ubunge wa CCM,jimbo la Kalenga,Ndugu Godfrey Mgimwa,huku shangwe na vifijo vikiwa vimetawala eneo hilo pasina kujali mvua kubwa ilioyokuwa ikiendelea kunyesha eneno hilo.
 Pamoja na Mvua kubwa iliyokuwa inanyesha katika kijiji cha Wenda kata ya Mseke-Iringa Vijijini,wanakijiji wa eneo hilo walionekana kuvutiwa mno na sera za mgombea ubunge wa CCM,Godfrey Mgimwa alipozungumza nao kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.Kama uonavyo pichani baadhi ya Wanakijiji wakilikimbiza gari ya mgombea huyo mara baada ya kumaliza mkutano wake.Mgombea huyo aliwaomba wampigie kura za ndio na kumpa ridhaa ya kuwaongoza kama Mbunge wa jimbo hilo,ili wayamalizie yale yaliyokuwa yameachwa na Mbunge aliyekuwepo hapo awali,Marehemu Dk Willliam Mgimwa.

Chanzo:- michuzijr

No comments:

 
 
Blogger Templates