Pichani shoto ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,Ndugu,Jerry Silaa wakishangilia jambo kwa pamoja na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga kwa tiketi ya chama cha CCM,Ndugu Godfrey William Mgimwa,katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika jana kwenye uwanja wa shule ya msingi Katenge katika kijiji cha Mgama,kata ya Mgama,Iringa Vijijini.
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,Ndugu,Jerry Silaa pichani kulia akizungumza mbele ya wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla waliofika kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika jana kwenye uwanja wa shule ya msingi Katenge katika kijiji cha Mgama,kata ya Mgama,Iringa Vijijini.Jerry Silaha amewataka wananchi na wakazi wa kijiji hicho kumpigia kura ya ndio ifikapo machi 16,Ndugu Godfrey Mgimwa ili aweze kuliongoza jimbo la Kalenga na kuyaendeleza mambo yote yaliyoachwa na Mbunge aliyepita.
Mwenyekiti wa CCM mkoa Iringa,Bi.Jesca Msavatavangu akizungumza mbele ya Wanachama wa chama hicho na Wanachi kwa ujumla kwenye mkutano wa kampeni wa uchaguzi mdogo Jimbo la Kalenga, katika kijiji cha Mgama kata ya Mgama,Iringa Vijijni akimpigia debe mgombea ubunge wa jimbo hilo,Ndugu Godfrey Mgimwa.
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,Ndugu,Jerry Silaa pichani kulia akizungumza jambo na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga kwa tiketi ya chama cha CCM,Ndugu Godfrey William Mgimwa,katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika kwenye kijiji cha Ibumila kata ya Mgama,halmashauri ya Iringa vijijini mkoani Iringa.Jerry Silaa amewaomba wana Ibumila na wana Kalenga kwa ujumla wake kumchagua Godfrey Mgimwa ili kukamilisha mipango mbalimbali aliyoiacha na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Marehemu Dk.William Mgimwa.
Kada wa CCM,Ndugu Fredrick Mwakalebela akimpigia debe mgombea Ubunge wa jimbo la Kalenga,kupitia chama hicho,Ndugu Godfrey Mgimwa katika kijiji cha Mgama kata ya Mgama,wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini humo.
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,Ndugu,Jerry Silaa akipeana mkono na Mwenyekiti wa CCM mkoa Iringa,Bi.Jesca Msavatavangu mara baada ya kumaliza kumuombea kura mhombea Ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia CCM,Ndugu Godfrey Mgimwa.
Mwenyekiti wa CCM mkoa Iringa,Bi.Jesca Msavatavangu akizungumza kwenye mkutano wa kampeni wa uchaguzi mdogo Jimbo la Kalenga, katika kijiji cha Mgama kata ya Mgama,Iringa Vijijni akimpigia debe mgombea ubunge wa jimbo hilo,Ndugu Godfrey Mgimwa.
Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga,kupitia CCM,Ndugu Godfrey Mgimwa akiwa emakalishwa kwenye kigoda mara baada ya kuvalishwa mgorole wa kimila kwama ishara ya heshima na kumtakia ushindi wa kishindo,mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Mgama kata ya Mgama wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini hapo jana.
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,Ndugu,Jerry Silaa pichani kulia akizungumza mbele ya wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla (hawapo pichani) waliofika kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika jana kwenye uwanja wa shule ya msingi Katenge katika kijiji cha Mgama,kata ya Mgama,Iringa Vijijini.Jerry Silaha amewataka wananchi na wakazi wa kijiji hicho kumpigia kura ya ndio ifikapo machi 16,Ndugu Godfrey Mgimwa ili aweze kuliongoza jimbo la Kalenga na kuyaendeleza mambo yote yaliyoachwa na Mbunge aliyepita.
Chanzo:- michuzijr
No comments:
Post a Comment