Kata ya Bagamoyo ni miongoni mwa kata 23 za Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Kata hii iko katikati ya mji wa Tukuyu ambako ndiko makao makuu ya wilaya ya Rungwe yako, katika miaka minne nyuma hali ya kata ya Bagamoyo ilikuwa mbaya sana katika maeneo mengi ikiwemo majengo ya ofisi za Serikali, ufaulu wa wanafunzi katika Shule za Msingi, Miundombinu ya barabara n.k
Baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 wananchi wa kata ya Bagamoyo walimchagua Ndugu Bashiru Madodi kuwa Diwani wao, katika kipindi kifupi diwani wa kata ya Bagamoyo akishirikiana na wakazi wa kata hiyo wameanza kuibadili sura ya kata hiyo kama picha hapa chini zinavyoonyesha.
Jengo jipya la ofisi ya Kata ya Bagamoyo kama linavyoonekana kwa mbele likiwa katika hatua za mwisho za umaliziaji wa ujenzi. Kazi hii inafanywa na Diwani wa Kata hiyo Mhe. Bashiru Madodi
Jengo jipya la ofisi ya Kata ya Bagamoyo kama linavyoonekana kwa nyuma.
Picha ya jengo la ofisi ya Kata ya Bagamoyo ambalo Diwani Madodi alilirithi kutoka kwa Diwani aliyemtangulia. Mara baada ya kuchaguliwa Mhe Madodi alilibomoa lote na kuanza ujenzi upya
Hali ya jengo la zamani lilivyokuwa kwa nyuma
Hakika jengo hili lilikuwa limechakaa sana na halikustahili kuwa ofisi ya Serikali kama linavyoonekana
Nuru mpya ya Kata ya Bagamoyo, Jengo la kisasa kabisa.
Picha na habari na
Basahama Blog
No comments:
Post a Comment