Social Icons

Wednesday, 30 April 2014

JE, UTAJIRI WA NCHI NDIO FURAHA YA WANANCHI?

Mafuta na gesi yameiletea nchi ya Qatar utajiri mkubwa kiasi kwamba , wanaweza kutumia dola billion mia mbili 200 kwa ujenzi wa viwanja vya michezo na miundo mbinu kwa maandalizi ya kombe la dunia la mwaka wa 2022.

Lakini mali hii isiyo na kipimo imeiletea nchi ile furaha?

Serikali ya Qatar imelata mageuzi ya haraka katika nchi ambayo umaskini ulikuwa umekithiri pakubwa chini ya mwongo mmoja tu uliopita. Sasa Qatar imekuwa nchi yenye utajiri mkubwa zaidi duniani.

Jambo ambalo wengi hawajalielewa na athari yake ya mabadiliko ya haraka kiasi hiki kwa watu wa Qatar.

Unaweza kuhisi shinikizo katika mji wa Doha.

Mji mzima umejaa wajenzi na mijengo ambayo bado inaendelea kujengwa huku majumba mengi hata kufikia wilaya nzima yakiwa yamebomolewa ili kuboreshwa.

Maisha kwa waqatari wengi ni mazuri

Msongamano mkubwa wa magari kila mara ukizidi kuongeza masaaa ya kufanya kazi kwa siku.

Wananchi wa Qatar wananufaika na masomo ya bure, huduma za afya bila malipo, hakikisho la ajira, misaada kwa ajili ya makazi pamoja na maji na umeme bila malipo. Hata hivyo ukwasi wa aina hii umezua changamoto zake.

Vyombo vya habari katika nchi hiyo vinaripoti kuwa kufikia asilimia 40 ya ndoa zinavunjika huku zaidi ya thuluthi tatu ya watu wazima kwa watoto wakiwa wanene kupita kiasi.

Daktari Kaltham Al Ghanim ambaye ni mhariri wa sosholojia katika chuo kikuu cha Qatar anasema kuwa maisha ya kijamii na kiuchumi yamebadilika na kuathiri pakubwa familia ambazo sasa zinatengana na watu kusalia wakiwa watumizi tu bila ya kutafuta.

Katika jamii ambayo wahamiaji wa nchi zingine wamewazidi watu wa Qatar kwa takriban wageni saba kwa kila mQatari, kuna ongezeko kubwa la malalamiko miongoni mwa wanafunzi wanao hitimu kutoka kwa vyuo vikuu.

Wana lalama kupewa kazi zisizo na hadhi huku zile za kuridhishwa zikipewa wahamiaji.

Majengo ya kifahari ya Qatar

Kuna hisia kali kuwa katika mchakato wa kung’ang’ani maendeleo, jambo ambalo ni la muhimu kwa waQatari limehujumiwa.

Maisha ya jamii za Qatari yanatamausha huku watoto karibu nchi nzima wakilelewa na yaya kutoka nchi za nje kama vile Ufilipino, Nepal au Indonesia.

Jambo ambalo linafungua upungufu wa utamaduni na mtazamo kati ya vizazi. Mama mmoja mwenye umri wa miaka 60 Umm Khalaf anasema kuwa wakati wa ujana wake watu walikuwa ni wabunifu na ni jambo lenye uchungu kuupoteza ule urafiki na umoja wa familia.

Watu wengi wanakubaliana kuwa wanasiasa wamejitenga na mahitaji ya watu, hasa katika swala hili la kutaka kuleta kombe la dunia la mwaka wa 2022 nchini Qatar mchakato ambao umekumbwa na madai ya ufisadi. Pia kule kufuatiliwa kwa karibu na vyombo vya habari kumesababisha kuongezeka kwa ujenzi.

Katika nchi yenye sheria kali zinazo wafanya wahamiaji wa kigeni pale kidogo kama watumwa pamoja na kuanguka kwa washirika wake wa Eneo hilo ikiwepo Saudi Arabia na majirani wengine, huenda serikali ya Qatar ikajipata na Shinikizo zaidi la kubadili sheria zake huku ikitazamia kombe la dunia ambalo bado lina miaka nane kabla halijachezwa pale.

Chanzo: bbc

No comments:

 
 
Blogger Templates