Social Icons

Sunday, 20 April 2014

Makanisa takriban 20 hufungwa ama kuuzwa kila mwaka nchini Uingereza

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu


Kanisa la Mtakatifu John lililopo Blackpool Uingereza, lilijengwa mwaka 1844, bado linavutia.


KWA TAARIFA YAKO hii leo tupo nchini Uingereza, moja ya taifa ambalo limesifika kupeleka wamisionari sehemu mbalimbali duniani kuhubiri habari njema za Yesu Kristo na habari hizo kuwafikia vyema wapelekewaji ambao wengi wao wamebadilisha maisha yao na kuamua kumfuata Kristo. Mbegu ya Waingereza hao imefanya kazi njema ambayo imezaa matunda bora ambayo hata sasa ni ushahidi katika mataifa hayo kwakuwa injili ya Kristo imesimama mpaka leo.

KWA TAARIFA YAKO pamoja na taifa hilo kuwa nambari wani katika kusamabaza injili ya Kristo, lakini kwasasa mambo ni tofauti katika taifa hilo ambalo awali misingi yake ilijengwa katika Kristo nasasa ni mabadiliko makubwa kwani asilimia 70 ya wakazi wa nchi hiyo kwasasa hawaamini uwepo wa Mungu, zaidi ya kuamini mambo ya kisayansi jambo ambalo limesababisha hata mahudhurio makanisani ni hafifu hususani kanisa Anglikana ambalo ndio kanisa mama nchini humo ambalo naweza sema ni kanisa ambalo lina majengo mazuri sana yaliyotunzwa toka enzi hizo mpaka sasa yakiendelea kuwa na mvuto wa kipekee ndani na nje ya majengo hayo. 

KWA TAARIFA YAKO kwa mujibu wa taarifa kutoka katika moja ya vyanzo vya habari vya kanisa Anglikana la nchi hiyo ni kwamba takribani makanisa 20 hufungwa kila mwaka na majengo yake kugeuzwa kwa matumizi mengine kulingana na mnunuaji anavyoamua ama mkodishaji wa jengo, pamoja na wananchi wasehemu husika. KWA TAARIFA YAKO jambo hili limekuwa lakawaida sana kwa miaka ya karibuni katika nchi hiyo, ambapo makanisa ambayo hufikiriwa kufungwa hupelekwa wachungaji katika makanisa hayo ili kuvuta watu kuja kusali endapo lengo halitatimia la watu kuitikia mwito basi kanisa hilo hufungwa na jengo kuingizwa mnadani chini ya usimamizi wa kanisa kwa matumizi mengine lakini pia mtumiaji wa jengo hutakiwa kulitunza kwa ajili ya kumbukumbu ya vizazi vijavyo kama ilivyoada ya Waingereza. 


Kanisa kuu Anglikana maarufu, la Durham Cathedral lenye miaka takribani 1000 toka lijengwe bado imara na linavutia wengi.©Wikipedia
KWA TAARIFA YAKO katika kufanya juhudi za kuwarejesha waumini kanisani, dayosisi za kanisa hilo hufanya maarifa wanayodhani yakazaa matunda, moja wapo ni kanisa la Mtakatifu Margaret lililopo King's Lynn waliamua kufungua mgahawa wa McDonalds kanisani hapo ili kuvutia vijana na waumini wengine kurudi kanisani, lakini pia kama haitoshi kuna makanisa ambayo hayapo mbali na baa ili kuwapa fursa waumini wake wanaopenda kutumia vileo kuingia katika baa hizo baada ama kabla ya ibada.


Kanisa likiwa na bango la Mgahawa wa McDonalds yote haya ili kuvutia waumini.
KWA TAARIFA YAKO wiki iliyopita nilihudhuria ibada ya kumuaga mchungaji msaidizi katika kanisa ninalosali maeneo ya Kensington magharibi mwa jiji la London, mchungaji huyu amekuwepo kanisani hapo kwa miaka mitano na ndiye alikuwa mshauri wangu wa kiroho hasa baada ya kufahamiana naye kwamba aliwahi kuishi Tanzania kwa miaka kadhaa, lakini pia kama haitoshi ni kati ya watumishi ambao wanamwamini Kristo, mchungaji huyu amehamishiwa huko Hastings kwakuwa kuna kanisa ambalo linahitaji mwamko kiupya hasa kutokana na kuwa na waumini 30 tu tena ni wazee ambao ibada zao zinaendeshwa kitamaduni zaidi. KWA TAARIFA YAKO lengo la mchungaji huyo kuhamishiwa huko ni kuokoa kutofungwa kwa kanisa hilo, endapo basi mwitikio utakuwa mzuri (kitu ambacho GK inakiombea kwamba Mungu akatende jambo) kanisa hilo halitafungwa.


Kanisa la Mtakatifu Bartholomew's katika mnada. soma orodha ya makanisa yanayouzwa kwasasa chini
KWA TAARIFA YAKO mdau wa GK unapopata taarifa kama hizi ni wakati wako wewe kulikumbuka taifa hili katika maombi maana baada ya miaka michache ijayo endapo mambo hayatabadilika basi utakuja kusikia asilimia 90 ya makanisa yote yamefungwa na majengo yanatumika kwakazi nyingine. Omba kwamba Mungu akafufue kazi yake kwa upya katika nchi hii ambayo kwasasa wachungaji na wahubiri kutoka Afrika ndio wenye makanisa makubwa ya kiroho ambayo waumini wake pia asilimia 90 ni kutoka Afrika ama visiwa vya karibeani.

Kanisa la Durham Cathedral ambalo GK liliwahi kupata nafasi ya kuabudu katika ibada ya usiku mtakatifu mwaka 2010 ©wikipedia.
Ifuatayo ni orodha ya makanisa yaliyowekwa kwenye tovuti ya kanisa Anglikana Uingereza tayari kuuzwa mwaka huu.

DioceseLocationNameContact
ManchesterBacup, LancashireBacup St JohnPeter Townley
ManchesterOn Rishton Lane to the south of Bolton town centre (BL3 2BN)Bolton le Moors St Simon and St JudeLongden and Cook Commercial
ManchesterJust off Bury New Road (A56) close to Great Clowes StreetBroughton St JohnLongden & Cook Commercial
Exeter1.5 miles north of outskirts of City of ExeterCowley St AnthonyToby Perry
DurhamMiddleton St George, Darlington, DL2 1APSt Laurence’s Church, Middleton St GeorgeGSC GRAYS
ManchesterOn St James’ Street in Farnworth, Bolton (BL4 9SJ)New Bury St JamesLongden and Cook Commercial
ManchesterSmallbridge, Rochdale, LancashireSmallbridge St JohnPeter Townley
TruroTregolls Road, Truro TR1 1ZQTruro St PaulMr Duncan Ley
ChichesterAthelstan Road, Hastings TN35 5JEHastings All SoulsOliver Dyer
WorcesterSt Georges Road, Redditch B98 8EERedditch St George the MartyrA. Victor Powell (Chartered Surveyors)
York





Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO kwa leo vinginevyo tukutane wiki ijayo.
Acklam Road, Thornaby, Stockton-on-Tees, Cleveland TS17 7HBThornaby St LukeGCS Grays (ref Calum Gillhespy)





No comments:

 
 
Blogger Templates