Social Icons

Friday, 18 April 2014

Mjadala huu nimeukuta Face book naomba nawe upitie kuhusu Zanzibar na kuhujumiana


1: Mtoa hoja wa kwanza:

Mzee Jumbe alipinga Muungano hamna mtu asiyejua hapa kilichomkuta pale Mji Mwema;Mzee Jaji Dourando aliupinga Muungano akawekwa kizuizini nchini Ghana;Dr Othman Ally Mpemba na  mmoja wa madaktari bingwa wa kwanza TZ mpinga mfumo huu wa Muungano alikamatwa na maafisa usalama akiwa kazini kwake Mbeya Hospital na hadi leo hajulikani alipo!Mzee Dr Khasim Hanga aliyekuwa Waziri Kiongozi wa kwanza ZNZ aliupinga Muungano huu maafisa usalama wakamkamata na kumtia kizuizini gereza lenye mateso la Kiinua Miguu kabla ya kupotea asijulikane alipo hadi sasa ingawaje familia yake inaomba waonyeshwe hata kabuli lake tu!Mzee Mwafongo wa Tukuyu yy aliwekwa kizuizini kijijini kwake Lufilyo na kunyang'anywa kila kitu hadi watoto wake!Hizi ni facts kaka zangu George Mwakalinga na Christopher Thomas Mullemwah na hamuwezi zibadili!Nyerere angeishi hadi leo angefikishwa The Hague-Uholanzi kujibu mashtaka ya ukatili dhidi ya raia wake!Kumkosoa Mwl Nyerere ilikuwa inajitakia ukaozee Ukonga!Yaliyomkuta Mzee Kambona au Mama Titi hayavumiliki ukiyasoma!

2: Mtoa hoja wa pili:

Charles, Waliomfikisha Jumbe mpaka kung'olewa Dodoma ni Wazanzibari wenzake wa kikundi cha Frontliners kikiongozwa na Sharif Hamad. Yeye Jumbe akiongoza kundi lingine la Liberators ambao ndio wengi alifukuzwa nao pamoja mwaka 1984.

Vita vya hayo makundi ndio vilimfikisha Jumbe hapo alipo. Wakati huo Jumbe na kundi lake wanataka serikali tatu na Hamad na kundi lake wanaunga mkono muundo uliokuwepo. Jumbe alitaka madaraka Zaidi Zanzibar ili awe na nguvu ya kuwashughulikia akina Hamad, badala nzuri wenzake wakamuwahi. Sijui Lissu halijui hili maana kama ni watu kubadili misimamo wako wengi sana.

Hanga aliuawa na Wazanzibari wenzake wala sio Nyerere. Kosa la Nyerere lilikuwa kumrudisha Zanzibar kwenda kukabiliwa na mashitaka. Lakini alijifunza kutokana na hilo kosa na ndio maana baadaye hakuwarudisha akina Salim na hata babu.

Lissu atawachanganya vijana ambao hamjui historia ya nchi yenu. Nyerere hakuishi kwa kudanganya na Uwongo na alitujengea taifa lenye heshima na ambalo wengi wetu tumeishi kwa kuheshimiana.

3: Mtoa hoja wa tatu:

kwahiyo maalim seif alihusika kumuangamiza jumbe? eti mullemwah! sharif ahmad huyu makamu wa rais? hawa waliomchagua ilikuaje sasa hawatambui historia yao? kumbe maadui ndio hao viongozi wao haya madai yasiyo kwisha wanatumia kuficha udhaifu wao? sasa tundu lissu mbona amezungumza mambo ya kawaida tu kwanini mnaongeza tafsiri zenu? yeye anazo sababu za kumuita nyerere muongo wewe unapinga nini sasa? kwani akili zako na za lissu ni sawa?


4: Mtoa hoja wa nne:

Mnachanganya habari hapa akina Christopher Thomas Mullemwah na George Mwakalinga!Someni vyema historia ya Frontliners nani alikuwa anakiunga mkono!Maalim Seif na Nyerere walitengana baada ya Nyerere kumgeuka Maalim na kuanza kumuunga mkono Mzee Idris Wakil kwenye uchaguzi mkali baada ya Jumbe kufukuzwa!Hapo Dodoma kuna Mzee mmoja anaitwa Abubakr Khamis alikuwa Mwanasheria Mkuu ZNZ aliyefukuzwa na akina Maalim mwaka 1988!Chris mtafute Mzee huyu uchote hekima zake!Yaliyompata Mzee Kasanga Tumbo je?

Basahama blog

No comments:

 
 
Blogger Templates