[AHMED Z. MSANGI – SACP] KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
WATU WAWILI WANAFUNZI WA MWAKA WA KWANZA DIPLPOMA YA BUSSINESS ADMINISTRATION CHUO CHA MZUMBE KAMPASI YA MBEYA, WAKAZI WA FOREST YA ZAMANI HOSTELI ZA NJE WALIOTAMBULIWA KWA MAJINA YA 1.MICHAEL TARIMO (20) NA 2. ALBERT SHENKALWA (23) WALIKUFA MAJI BAADA YA MTUMBWI WALIOKUWA WANAUTUMIA KUPIGWA MAJI, KUPINDUKA NA WAO KUSHINDWA KUOGELEA. TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 02.05.2014 MAJIRA YA SAA 15:00 ALASIRI HUKO KATIKA ZOO YA WANYAMA ILIYOPO KATIKA HOSPITALI TEULE YA IFISI – KATA YA SONGWE, TARAFA YA BONDE LA USONGWE, WILAYA YA MBEYA VIJIJIJINI. WANAFUNZI HAO WAKIWA NA WENZAO 12 WALIKWENDA ENEO HILO KWA AJILI YA PICKNIC NA KUANGALIA WANYAMA NA BAADAE KWENDA KWENYE BWAWA LINALOTUNZA SAMAKI NA KUANZA KUINGIA NDANI YA BWAWA HILO KWA KUTUMIA MTUMBWI HUO KWA ZAMU. KATIKA BWAWA HILO WATU HAWARUHUSIWA KUOGELEA ISIPOKUWA KUINGIA KWA MTUMBWI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMEDI Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUWA MAKINI NA MAZINGIRA WANAYOKWENDA KUTEMBMELEA ILI KUEPUSHA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA. |
No comments:
Post a Comment