Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili katika shule ya sekondari ya Kiwele kata ya Kitunda wilayani Sikonge mkoa wa Tabora ambapo amekagua miradi mbalimbali ya nyumba ya walimu na maabara zinazojengwa katika shule hiyo, Kinana akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi pia amekagua majengo ya kituo cha afya cha Kitunda, katika ziara hiyo mganga mkuu wa kituo hicho Dk.Silvanus Kabutula amelalamikia kuchelew kwa ujenzi wa jengo la upasuaji na kujifungulia akina mama wajawazito jambo ambalo linasababisha matatizo makubwa kwa wakazi wa kata hiyo na vijiji vya jirani ambavyo vinategemea huduma kutoka katika kituo hicho.
Akitolea ufafanuzi zaidi kuhusu suala hilo mbunge wa jimbo la Sikonge Mh. Said Mkumba amesema, mkandarasi wa ujenzi wa vituo hivyo ameshindwa kumaliza kazi kwa wakati na mkataba ulianza 28/ 10/2009 na ulitakiwa kumalizika 2/5/2011 lakini mpaka sasa vituo hivyo na zahanati havijakamilika jambo ambalo linakwamisha ustawi wa jamii katika suala zima la afya, Ameongeza kuwa kupitia mradi wa Mradi wa kupunguza vifo kwa akina mama Support to Martenal Mortality Project Reduction (SMMRP) jumla ya vituo saba vya kutolea huduma wilayani Sikonge vilitakiwa kujengwa ambavyo ni Kipili,Kitumbi,Tumbili, Pangale,Kitunda, Mazinge na Kisanga ambapo jumla ya shilingi bilioni 2,051,723,850 zimelipwa kwa mkandarasi huyo hata hivyo kazi hiyo jaijakamilika mpaka sasa, Kuhusu za la Tumbaku Mkumba amesema wakulima wa tumbaku waruhusiwe kuuza tumbaku wanapotaka kwa sababu vyama vya ushirika vya msingi vinawadhulumu wakulima hao.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ameahidi kufikisha kwa suala hilo kwa Mh. Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kilio cha wananchi wa Sikonge kuhusu suala la zahanati hizo kutokumalizika kwa wakati na matatizo ya wakulima kutolipwa fedha zao za mauzo ya tumbaku kwa wakati.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-SIKONGE-TABORA)
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akiwasili katika shule hiyo.
No comments:
Post a Comment