Akiongea katika kipindi cha BBC asubuhi, mwanafunzi wa kike Mtanzania anayesoma mashariki mwa Ukraine ameilalamikia serikali ya Tanzania kwa kuwatelekeza katika uwanja wa mapambano Licha ya kuomba msaada kwa Serikali, ili iwasaidie kuondoka katika eneo hilo hatari kwa maisha yao, lakini mpaka sasa hakuna majibu yoyote waliyoyapata kutoka Serikalini.
Akiongea kwa uchungu Mtanzania huyo amesema wenzao Wakenya wametumiwa usafiri na kurudishwa nchini kwao, na wanafunzi wanaotoka nchini Uganda wamehamishiwa katika mji ambao ni salama na kupangiwa nyumba za kuishi, lakini Watanzania wameachwa katika uwanja wa mapambano eneo ambalo linashuhudia siraha za kisasa na nzito zikitumika na kuhatalisha usalama wa maisha yao.
Swali la kujiuliza ni kweli viongozi wa Tanzania wameamua kuwatoa sadaka Watanzania wenzetu kwa kuwaacha katika uwanja wa vita bila ya msaada wowote?
Je, kungekuwa na mtoto yeyote wa kiongozi wa Tanzania katika eneo hilo, viongozi wetu wangekaa kimya na kuacha apoteze maisha, au ni kwa sababu walioko huko ni watoto wa Watanzania wasio viongozi wa Serikali?
Sisi wana Basahama blogspot tunawaomba viongozi wa Serikali ya Tanzania kuchukua hatua za haraka kuwaondoa Watanzania wenzetu walioko kwenye eneo hatari la uwanja wa vita nchini Ukraine.
Basahama blogspot.
3 comments:
SIKIA KWA JILAN HUSIOMBE
SIKIA KWA JILAN
SIKIA KWA JILAN
Post a Comment