Leo katika mwendelezo wa vivutio hivyo vya Utalii katika Mkoa wa Mbeya tutakiangazia kivutio kimoja wapo ambacho ni Maporomoko ya Kaparogwe, Maporomoko haya ni moja ya Kivutio kikubwa cha Utalii Nchini Tanzania ambacho kinavutia sana.
Maporomoko haya ambayo yapo Kilometa 11 kutoka Ushirika Tukuyu sehemu ambayo kuna barabara nzuri na Gari la aina yoyote inaweza kufika katika kivutio hicho.
Kikosi kazi cha Mbeya yetu tulifika eneo Hilo na kujionea wenyewe eneo hilo na kujionea Maliasili hii na eneo ambalo kwa hakika linahitajika kusapotiwa na kulitangaza ili Dunia ipate fahamu kuwa kuna eneo kama hilo na wanahitaji kufika na Kutembelea.
Hivi ndivyo Safari yetu ilivyokuwa.. Fuatilia hapa
Haya ndiyo Maporomoko ya Kaporogwe yanavyo onekana kwa ukaribu kabisa
Hii ni njia yakuelekea Maporomoko ya Kaporogwe Utalii wa ndani baadhi ya watu wanaelekea katika Maporomoko ya Kaporogwe
Huu ni upande wa kuingilia kwa mbali ndivyo maporomoko yanavyo onekana
Kama kawaida unapotembelea maeneo kama haya lazima upate ukodaki wa kumbukumbu hapa kila mmoja akichukua matukio
Kwa hakika Joseph Mwaisango Mwandishi Mkuu wa Mbeya yetu akiwa mwenye furaha alipofika katika maporomoko haya ya kaporogwe mara baada ya kujionea yeye mwenyewe. Hapa ni eneo la Ndani kabisa ya Maporomoko hayo.
Hili ni Moja ya eneo la Mapumziko, watu wanaofika huja hapa na kukaa kisha kutazama uzuri wa Maporomoko ya Kaporogwe Maji yakiwa yanashuka kwa kasi katika maporomoko ya Kaporogwe
Kwa Jirani kabisa Maji yanavyomwagika katika Maporomoko ya kaporogwe
Unaweza ukaona maajabu sana lakini hii ndio njia ya kuingilia maporomoko ya kaporogwe
Head of Group Research and Product Development wa Tone Multimedia Group ambao ni Wamiliki wa Mbeya yetu Blog Fredy Anthony Njeje akiwa chini kabisa ya Maporomoko ya Kaporogwe kujionea jinsi maji yanavyo mwagika, katika eneo hili la chini kuna hali ya unyevu vyavu na baridi ya aina yake ambayo haiumizi lakini inayohamasisha kuendelea kuwepo katika eneo hilo muda wote.
Hii ni Barabara inayotokea eneo Linaitwa Kissa kuelekea katika Maporomoko ya Kaporogwe Mwandishi Mkuu wa Mbeya yetu Blog Joseph Mwaisango wa Kwanza kulia akiwa na wenyeji wanaokaa maeneo ya Maporomoko ya Kaporogwe.
Wa kwanza kulia ni Fredy Anthony Njeje akiwa pamoja na wakazi wanaoishi maeneo ya Kaporogwe Barabara iliyojengwa na Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe inayoelekea kwenye Maporomoko ya Kaporogwe.
Chanzo: Mbeya Yetu blog
2 comments:
Mwenyezi akiniwezesha one day yes ntafika
One day yes akiniwezesha sir muumba
Post a Comment