Social Icons

Thursday, 11 September 2014

HADITH: Missed call ya shemeji -10


“Nasema mwenzio nimenasa ujauzito, maana nimepitiliza.” “Una maana gani?”
“Nina ujauzito wako bwana, acha mambo yako wewe.” SONGA NAYO…
He! Shemeji! Una unini wangu?”
“Ujauzito.”

“He! Kwa hiyo?”
“Kwa hiyo nini shemeji, wewe si ndiye mhusika!”
“Ina maana upo tayari kuzaa?”
“Tatizo liko wapi?”
“Kuzaa na mimi?”
“Mimi sioni shida.”

“Ukitoa mtoto yupo kama mimi mtupu?”
“Haiwezekani hata siku moja.”
“Mh! Hapana, tutoe shemeji.”


Kutoa! Sisi tuliapishwa na baba, mtu akipata mimba akitoa anakufa, hajakwambia mkeo?” alisema dada wa Aisha huku akijing’atang’ata midomo.
Beka hakuwa tayari kuzaa na shemeji yake huyo hata kama walikubaliana kula uroda. Kwake kuzaa na shemeji yake ilikuwa ni kupitiliza kwa kufuru jambo ambalo aliamini linaweza kumpa wakati mgumu katika maisha  ya kifamilia…

“Yaani shemeji itakuwa ngumu sana wewe kuzaa na mimi halafu…”
“Hata mimi itakuwa ngumu sana kutoa hii mimba. Hivi  kama ulikuwa hutaki kuzaa na mimi kwa nini hukuniambia mapema?”
“Shemeji kwani hukujua?”
“Kwamba?”

“Mimi na wewe hatuwezi kuzaa!”
“Tunaweza, sii hutaki! Au hatuwezi kivipi wakati mimi tayari nina mimba yako.”
Beka aliangalia pembeni, shemeji yake akamfuata na kumshikashika sehemu mbalimbali za mwili na kumfanya Beka kusisimka…

“Una…jua she…m tati…zo wewe hu…jui tu, mdo..go wako…ana…” alisema Beka huku akisisimka mwili kutokana na kushikwashikwa na shemejiye mwilini. Alihisi kuchanganyikiwa.

Shemeji mtu huyo naye alijua Beka ameshaingiliwa akili hivyo akazidisha kujituma ili kuingia kwenye hatua nyingine na kuisahau ile ya kwanza ya madai ya mimba…
“Shemeji…”
“Mmh!” Beka aliitika kwa sauti ya chini sana huku macho yakiwa hayaoni sawasawa.
“Unataka nini?”

“Unataka unipe nini wewe?”
“Chochote unachokitaka wewe.”
“Sawa na wewe nipe chochote unachotaka kunipa.”
Mazungumzo yote hayo yaliendelea huku kila mmoja akiwa tayari amewaka moto, hakuna kitu mbele yao zaidi ya mahaba.

Shemeji alimvua nguo Beka huku wakiendelea kusemeshana maneno mbalimbali yenye kuhamasishana zaidi kimahaba mpaka wakajikuta wote hawana nguo kitandani wakaingia mechini..!

***
Ilikuwa siku ya Jumapili, Aisha alikuwa nyumbani, mumewe pia. Aisha alikuwa akizungumza na mumewe kuhusu mambo mbalimbali ya maisha, ghafla dada wa Aisha alikatiza mbele yao akitokea chumbani kwake kwenda bafuni huku akikimbia akiwa amejishika tumbo na kujipigapiga kifuani kama vile anasikia maumivu…

“Dada nini tena?” Aisha aliuliza akimfuatilia kwa macho.
Beka moyo ulimlipuka, alijua tayari kinakaribia kunuka kwani dalili zile za shemeji yake ni za ujauzito wa wazi kabisa…

“Ngoja niende nikamcheki dada,” alisema Aisha.
“Ukamcheki nini sasa wakati mtu mwenyewe anaonesha hataki kusema?”


Atasema tu, si ajabu anaumwa sana.”
Aisha alikwenda bafuni akakutana na matapishi kibao huku dada yake amechuchumaa…
“Dada, ni nini?”
“Naumwa.”
“Nini zaidi?”
“Nahisi malaria.”

“Malaria au mimba dada?”
“Malaria, mimba niitoe wapi mimi?”
“Dada angalia sana na safarisafari zako hizo, kapime dada.”
“Aisha, mbona unanikosea adabu dada yako. Maswali gani hayo kwangu?”
“Sahamani sana dada,” alisema Aisha huku akiondoka kurudi sebuleni.

***
Usiku wa manane, Beka aliamka na kukosa usingizi kabisa. Akaanza kukumbuka picha ya shemeji yake kupita mbio mbele yake na kukimbilia bafuni. Akakumbuka maneno ya mke wake baada ya kurudi bafuni…
“Ana nini?”

“Mh! Mi nahisi ni mjamzito huyu!”
“Yeye kasema mwenyewe?”
“Hajasema, anasingizia homa.”
“Labda ni homa kweli.”
“Homa si angetapika nyongo, huyu kanasa. Na hii yote ni matokeo ya safari zake za kutoeleweka, yamemkuta sasa.”

“Da! Shemeji naye kumbe yupo?”
Beka alijikuta mapigo ya moyo yakimwenda kwa kasi ya ajabu…


Ile mimba lazima itoke. Nikisema iendelee kubaki nitaumbuka,” Beka alijikuta akisema kwa sauti…
“Unasemaje Beka?” mkewe alimuuliza kwa sauti iliyotoka kuamka ghafla.
“Aaa! Nilikuwa naota tu.”
“Sasa kama kuota ndiyo unaota mimbamimba?”
“Sijaota mimba, nimeota miiba. Nimeota kuna rafiki yangu amechomwa na miba, sasa anataka kutolewa.”

“Tuambiane mwenzetu maana tayari humu ndani tuna mjamzito, isijekuwa unamuotea yeye.”
“Aaah! Wapi! Yaani mimi niote ndoto ya mtu mwingine?”
“Kwani haiwezekani?”

Mara simu ya Beka ilitoa mlio wa meseji kuingia, Aisha akashtuka na kuuliza…
“Nani huyo saa hizi?”
Beka pia alishtuka. Alijua kwa swali la mkewe ina maana akishaisoma meseji hiyo lazima aseme ni nani kaituma. Sasa je, kama itakuwa imetumwa na shemeji mtu?
“Sijui nani?” alisema Beka akitaka kupotezea kusoma…

“Hebu msome tumjue huyo anataka nini usiku huu na waume za watu?” “Je, unajua nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma kwenye Ijumaa, Siku ya Ijumaa.


Itaendelea


Chanzo Globalpublishers

No comments:

 
 
Blogger Templates