Social Icons

Thursday, 11 September 2014

HADITHI: Missed call ya shemeji -11


Beka, licha ya kujibalaguza ilifika mahali akajua amekwisha. Akili za haraka zilimwambia kwamba katika uzoefu wa kawaida, haijawahi kutokea akatumiwa meseji usiku na mtu, kwa hiyo aliamini ni dada wa mkewe tu huyo.

“Soma basi,” alirudia Aisha.
“Kaka Beka mambo? Asubuhi pitia kwa mzee Ismail uchukue ule mzigo wako. Mimi wajina.”
Beka alisoma meseji ya uongo kwa kuitunga kutoka kichwani kwake, mkewe akaamini lakini akamuuliza…

“Ni mzigo gani kwani?”
“Kuna boksi la tende.”
“Ooo! Halafu jana huyo wajina wako nilikutana naye pale msikitini, akasema nikupe hai.”
“Okey.”

Beka alipoisoma ile meseji sawasawa, iliandikwa na shemeji mtu na ilikuwa ikisema…
“Piga ua galagaza, alfajiri njoo chumbani uniamshe na joto lako tamu! Mwaaa…”

Kichwani alikasirika kidogo kwa vile aliamini shemeji yake huyo ana akili timamu kwa hiyo alijua ubaya wa kutuma meseji kama ile usiku tena akiwa kitandani na mke wake.
“Kichaa sana huyu shemeji,” alisema moyoni.
***
Saa kumi na moja na nusu, Beka alitoka chumbani kwake akiwa ndani ya bukta tu hadi sebuleni. Aliangalia kulia na kushoto na kubaini hali ya utulivu na amani, akanyata kwenda kwenye mlango wa chumbani kwa shemeji yake…

“Sijui mlango uko wazi?” alijiuliza baada ya kuufikia mlango huo. Alisita kwa muda mrefu hapo mlangoni kama vile alikuwa akijua ndani kuna mwanaume mwingine sasa alikuwa akimsikilizia.

“Lakini ni kwa nini moyo unasita sana kuingia? Kuna balaa nini? Na kama kuna baya ni kutoka kwa nani sasa? Mimi nadhani nisiingie,” alisemasema mwenyewe pale mlangoni lakini moyo wa kuingia ukashinda, akafungua mlango na kuzama chumbani.

Shemeji mtu alishtuka kuona mlango umefunguliwa, akainuka kutoka kitandani na kukaa kwa kunyoosha miguu.“Afadhali umekuja, baridi sana,” alisema shemeji mtu huyo huku akiwa hayumo ndani ya shuka wala kanga halafu eti anasema kuna baridi! Kivipi? Ilikuwa ni zaidi ya baridi.
Beka alipanda kitandani huku akisema…

“Lakini shemeji leo nimekuja huku najisikia uvivuuvivu sana, sijui kwa nini?”
“Hamna bwana, wewe unataka kuninyima joto,” alisema shemeji mtu huku akimparamia mume wa mdogo wake maana alianza kuhisi anamtolea visingizio ili amwache na njaa yake.

Walilala kiubavuubavu wakiangaliana. Wakaanza kushikanashikana mwilini huku wakinong’onezana maneno ya mahaba kama vile wao ni wana ndoa tena wako wenyewe tu.
Shemeji mtu ndiye aliyetangulia kupata moto wa mahaba, akamvutia kwake kijana huyo, wakaingia uwanjani na kuianza mechi kwa kasi na standadi.

Dada wa Aisha ilikuwa kama amedhamiria kumjulisha mdogo wake nini kipo kati yao kwani aliweweseka kwa sauti hadi kufumbwa mdomo ili sauti hiyo isitoke nje.
“Sasa shemeji kama ukisikika itakuaje? Si atakuja huku na kutukuta?” Beka alisema.

“Na mimi si mimi bwana, ni munkari wa mahaba umenipanda mwenzio.”
Maneno hayo pia aliyasema kwa sauti licha ya kwamba Beka alimtaka asipige kelele.
***
Aisha alishtuka kitandani na kukuta kweupe. Alishangaa!
“Huyu ameshaamka?” alijiuliza.

Alitega masikio ili kusikia kama mumewe aliingia chooni maana chumba chao kilikuwa ‘self contain’. Ukimya ulitawala hali iliyoashiria kwamba hakuwemo mle bafuni wala chooni…
“Baby…baby,” alijaribu kuita kwanza ili kujiridhisha.

Akatoka kitandani na kuifuata simu yake kisha akaitupia macho…
“Mh! Saa kumi na mbili na dakika tatu. Mbona si kawaida yake saa hizi awe nje!”
***
Beka na shemeji yake walipitiwa usingizi baada ya mzunguko wa kwanza wa mechi, wakalala kabisa. Hakuna aliyekuwa na habari na dunia inakwendaje!
Baby,” Aisha aliita sasa akiwa amefika sebuleni ambapo hakuona dalili yoyote kwamba mumewe alifika hapo…

“Baby,” aliita kwa sauti ya juu sasa, akashtuka kutoka kwenye chumba cha shemeji yake. Kidogo aitikie ‘sema’, kushtuka hivi kumbe alikuwa kwenye mchepuko.

“Mh! Shemeji tumefumwa,” alisema Beka, shemeji yake naye akashtuka…
“Mungu vile tumefumwa,” alisisitiza akitoka kitandani. Akavaa bukta yake na kwenda kuushika mlango. Aliposikia sauti inatokea sebuleni alirudi, akajishika kichwa na kuanza kujuta…

“Nilisema mimi, dalili zilishaonesha kwamba kuna balaa. Ndiyo hili sasa.”
“Beka,” Aisha aliita tena, sasa alibadili jina.

“Shemeji ingia chini ya kitanda,” shemeji mtu alimwambia Beka huku akifunua godoro, akabinyua chaga za upande mmoja. Beka alizama ndani yake, ile anamalizikia tu, Aisha akagonga mlango…
“Dada,” aliita kwa sauti iliyojaa utulivu.

Dada yake alirudisha chaga polepole kisha akafunika godoro vizuri  na kurudishia shuka kama awali…
“Dada.”
“Ee.”

“Samahani, nina shida.”
Je, nini kiliendelea 

Itaendelea

Chanzo Globalpublishers


No comments:

 
 
Blogger Templates