“Kha! Atakuwa nani ameweka?” nilijiuliza mwenyewe, nikauacha palepale, mimi nikapanda ngazi za kuingia ndani. Mlango ulikuwa wazi hali iliyoashiria kwamba, wenzangu walisharudi. Nilisukuma mlango, nikaingia. Nilikutana na harufu ya pafyumu, nikahisi walikuwa wakijiandaa kutoka.
Tuesday, 20 June 2017
SIMULIZI: Nilipanga nyumba moja na majini - 2
“Kha! Atakuwa nani ameweka?” nilijiuliza mwenyewe, nikauacha palepale, mimi nikapanda ngazi za kuingia ndani. Mlango ulikuwa wazi hali iliyoashiria kwamba, wenzangu walisharudi. Nilisukuma mlango, nikaingia. Nilikutana na harufu ya pafyumu, nikahisi walikuwa wakijiandaa kutoka.
SIMULIZI: Nilipanga nyumba moja na majini -1
Urusi: Shambulio la ndege ya Syria ni uchokozi
Urusi imeitaka Marekani kuheshimu uhuru na mipaka ya Syria baada ya kuangusha ndege ya jeshi la Syria katika mkoa wa Raqqa. Ndege hiyo ilikuwa katika harakati za kushambulia kundi linalojjita dola kiislamu IS.
Akizungumza katika mkutano wa mawaziri wa maswala ya kigeni mjini Beijing nchini China,waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov amesema shambulizi hilo na Marekani dhidi ya ndege ya jeshi la Syria huenda likazidisha mzozo nchini Syria na pia kuhatarisha vita dhidi ya ugaidi. Kisa hicho kimetokea wakati ambapo majeshi ya Syria yameimarisha mashambulizi yake dhidi ya wapiganaji wa IS kusini na magharibi mwa Raqqa, huku nalo jeshi la waasi wa Syria lijulikanlo kama Syria Democratic forces linaloungwa mkono na Marekani likiendeleza vita dhidi ya kundi kundi hilo la IS ndani ya mji wa Raqqa,ambao ndio ngome ya wapiganaji hao wa IS. Katika taarifa Marekani imesema ilichukua hatua za kujilinda baada ya majeshi hayo ya Syria kuangusha mabomu karibu na eneo linalosimamiwa na jeshi la waasi la Syria Democratic forces.
Marekani pia iliweka wazi kuwa haiyalengi majeshi ya Syria au Urusi, na iwapo muungano wa vikosi vyake utahitajika kufanya mashambulizi ya kujilinda basi havitasita kuchukua hatua.
Marekani inaunga mkono magaidi
Hata hivyo kamanda wa jeshi la Syria amelitaja shambulizi hilo dhidi ya ndege ya Syria kama ushahidi wa jukumu la Marekani katika kuunga mkono wapiganaji wa IS.Jeshi la Syria limeonya kutokea madhara makubwa kufuatia shambulizi hilo, na kusisitiza kuwa vitendo kama hivyo havitalizuia kuendelea na harakati zake za kupiga vita makundi ya kigaidi na kurejesha amani na usalama kwa wa Syria wote.Saa chache kabla ya kuangushwa kwa ndege hiyo ya jeshi ya Syria,
Marekani ilisema kuwa vikosi vinavyomuunga mkono rais wa Syria Bashar al-Assad viliwashambulia wanajeshi wa jeshi la waasi la Syria Democratic forces na baadhi yao kujeruhiwa. Mapema mwezi huu, Marekani iliangusha ndege isiyo na rubani ya serikali ya Syria, baada ya ndege hiyo kushambulia vikosi karibu na kivuko cha mpaka cha al-Tanf kwenye mpaka kati ya Syria na Iraq.Taarifa nyingine ni kuwa jeshi la Ukombozi la Iran limetoa onyo kali dhidi ya wapiganaji wa IS,na kusema mashambulizi yeyote dhidi ya Iran yatailazimisha kutumia nguvu zaidi.Tangazo hilo lilitolewa baada ya jeshi hilo la Iran kurusha makombora yaliyolenga kundi hilo la IS mashariki mwa Syria.
Chanzo. Dw.de
HADITHI; Niliolewa na Jini bila ya kutarajia - 12
NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA 12
Mara gafla nikaona mlango wa chumba changu ukifunguliwa, muda huo huo mkojo ulinitoka bila ya hodi.
Nilikuwa nangoja kuona huyo mtu wa ajabu atakayeingia ndani kwani nilijua kuwa kwa vyovyote vile siwezi kumkwepa.
Mlango wangu ulikuwa unafunguliwa polepole, ujasiri ukaniisha na kujifunika sura kwani sikuweza tena kutazama kitu kitakachoingia, mara nikashikwa kichwani na hapo nikapiga ukelele uliomuamsha hadi mama.
Mama akafika chumbani kwangu wakati mimi nikiwa bado nimeinama na kujikunyata.
"Vipi mwanangu jamani? Umepatwa na nini tena? Eti Penina, mdogo wako amepatwa na nini?"
Mama alimuuliza dada Penina ambaye naye alikuwa chumbani kwangu.
"Hata mimi namshangaa jamani, mi nilikuja chumbani kwake huku na nikafungua mlango taratibu ili nisimsumbue, shida yangu ilikuwa ni ile pochi ndogo. Nimeshangaa kumkuta hapo chini amejikunyata na kujiinamia nikaamua kumshika kichwani ili kumuangalia ana tatizo gani ila ile kumshika tu ndio akapiga makelele yote hayo.
Mama akaniangalia kwa makini,
"Kwani una nini Sabrina? Au kuna mambo ulikuwa unayawaza?"
Kitu cha kwanza kuwauliza ilikuwa ni muda,
"Kwani saa ngapi saizi?"
"Kumekucha mwanangu na dada yako ndio huyu amejiandaa kwenda kazini"
Nikabaki nashangaa tu na sikuelewa chochote, mama akaangalia chini na kuona yale majimaji ya mkoje.
"Kheee! Hadi umejikojolea Sabrina!! Ulikuwa unaogopa nini mwanangu?"
"Amejikojolea kweli loh"
Dada akaanza kucheka, kisha akachukua alichosema na kuondoka.
Nikabaki na mama tu pale ndani.
Kulipokucha vizuri nilikuwa nimeshaoga na kutafakari ya usiku kwakweli hakuna ambacho nilikuwa nakielewa. Nikaenda kwa mama jikoni kumuuliza,
"Nitaenda lini kwa kaka Deo mama?
"Sabrina mwanangu, umeanza uoga hadi wa kufikia kujikojolea si utaenda kutia aibu tu huko kwa kaka yako? Sidhani kama wifi yako atavumilia hali hiyo!"
"Mama yani bahati mbaya ya siku moja ndio unaihesabia kama siku zote? Mimi nataka kwenda kwa kaka haijalishi nini wala nini"
"Utaenda ila ndio hivyo utatutia aibu kama ukiendeleza hiyo tabia"
Nikamsikiliza mama ila moyoni bado nilitaka kwenda kwa kaka tu ili nibahatike kubadilisha mazingira kidogo.
Mchana nikajilaza sebleni kwani macho yangu yalikuwa mazito sana na kujawa na usingizi.
Mama akanishtua kuwa nimepata ugeni, kuamka nikamkuta ni Carlos ambapo mama alimkaribisha sebleni tayari.
Kisha mama akaenda chumbani kuendelea na mambo yake mengine, Carlos akaanza kujiongelesha pale.
"Mbona umechukia Sabrina? Hujaupenda ujio wangu?"
"Hapana, ila mbona umekuja bila taarifa?"
"Nimekuja kuangalia unaendeleaje Sabrina, nakujali sana mama angu. Nikwambie kitu Sabr."
"Niambie tu hakuna tatizo"
"Sabrina, wewe kweli ni binti mzuri na mrembo yani ingawa umetoka kulala ila bado unapendeza na kuvutia. Sura yako ina mvuto wa hali ya juu Sabrina, na umbo lako ni zuri sana ila samahani kama sifa zangu zimevuka mipaka.
Nikacheka na kumuangalia vizuri huyu Carlos ambaye leo alikuja na staili ya kunisifia.
Nikaamua kumuuliza swali Carlos,
"Mbona umeamua kunisifu kiasi hicho?"
"Anayestahili sifa acha apewe sifa yangu, kwakweli Sabrina hadi nimekupenda yani."
Nikashtuka na kumuuliza tena.
"Si unajua kama mimi nipo na Sam halafu tunapendana sana?"
"Tatizo lenu wasichana ndio hilo, mtu akitamka nakupenda basi wewe ushapelekea kwenye maana nyingine. Mimi nakupenda Sabrina kama Sabrina na si vinginevyo.
Nikabaki kimya kwani alinishushua, akaongea mambo mengine kisha akaondoka.
Nikawa naitafakari ile kauli ya Carlos ya kusema kuwa ananipenda Sabrina kama Sabrina na si vinginevyo, kauli yake bado ilikuwa na utata sana kichwani mwangu ila sikupenda kuijadili zaidi.
Jioni yake Carlos akanipigia simu na kuniuliza.
"Unapenda chocolate Sabrina?"
"Ndio nazipenda."
"Nikuletee?"
Nikasita kuitikia nikawa kimya tu na simu sikioni,
"Basi nakuletea"
Halafu akakata simu, nikawa nashangaa tu kwani bado sikuwa na imani nzuri na Carlos.
Haikuchukua muda nikamsikia Carlos akizungumza na mama.
"Mimi sio mkaaji mama, nimemletea Sabrina mzigo wake huu."
Kisha nikamsikia akiaga, baada ya muda kidogo mama akaniita huku akiufungua ule mzigo.
"Mmh kumbe chocolate, huyu ndio mkwe bwana sio huyo Sam wako."
Akafungua moja wapo na kuanza kula huku akinikabidhi ule mfuko, ila mimi nikakataa na kumuachia mama.
Dada yangu Penina nae aliporudi wakaungana na mama kula zile chokleti. Na mimi nikatumia mwanya huo kumchombeza mama,
"Leo mama tutalala wote eeh!!"
"Hakuna shida mwanangu tutalala tu, ila masharti yale yale kuongea na simu usiku sitaki."
"Sawa mama hakuna tatizo"
Nikatulia pale sebleni na kuwaangalia tu walivyokuwa wakisakamia zile chokleti huku wakisifu kuwa ni tamu sana.
Usiku ulipowadia, nilijipanga kulala na mama ila nilimkumbuka sana Sam nikaamua kumpigia simu kabla ya kulala ila haikupatikana.
Mawasiliano yangu na Sam yamekuwa yakisuasua sana kwa siku mbili tatu hizi hata nikishindwa kuelewa kuwa Sam atakuwa amepatwa na tatizo gani jingine.
Nikaenda kulala chumbani kwa mama ambaye alinisihi kuwa nisiwe muoga, kitu cha ajabu kwetu ilikuwa tunakumbuka vyote ila si kusali tena mara nyingine kukishakucha mama ndio anakumbuka kuwa hakufanya ibada.
Niliongea na mama pale mambo mawili matatu na kisha kulala.
Kama kawaida yule mkaka wa ndotoni alinitokea na kunifata mahali ambapo nilikuwa nimekaa katikati ya nyasi laini na nyororo, yule mkaka akaanza kusema.
"Nikupe kitu gani Sabrina ili ujue kama nakupenda? Nikuonyeshe ishara gani ili utambue upendo wangu kwako?
Nikawa namuangalia tu bila ya kumjibu chochote kile.
"Ninauwezo mkubwa sana wa kukufanya mke wangu hata kama hutaka ila mimi nahitaji ukubali kwa hiyari yako mwenyewe"
Akaanza kuongea maneno ambayo yalifanana na aliyoongea Carlos mchana.
"Sabrina, wewe ni binti mzuri na mrembo. Una sura ya kuvutia na umbo."
Kisha akamalizia kuwa.
"Anayestahili sifa apewe sifa yake"
Nikashtuka kutoka usingizini na kuhema juu juu.
Nikaanza kumfikiria Carlos, sura yake ikatembea mawazoni mwangu na ule ubaridi wa mikono yake nikaanza kuuhisi mwilini mwangu hadi kuanza kutetemeka.
Nikajiuliza maswali mengi sana juu ya Carlos, mara nikaona kivuli cha mtu mule chumbani kwa mama hapo sasa uoga ukanishika na kuanza kutetemeka, kile kivuli kikawa kinanisogelea taratibu yani kinakuwa kirefu nikawa nimemkumbatia mama na mara ikasogea hdi usoni kwangu na kunichekea.
Hapo sasa nikaanza kumuamsha mama kinguu ila mama alikuwa hoi kabisa hata hajitambui na hakuamka kabisa ikawa kama vile niko peke yangu mule chumbani.
Ikaanza sauti ya paka kama ile ambayo uwa inasikika chumbani kwangu, hapo nikazidi kutetemeka na kuzidi kumkumbatia mama.
Kwakweli leo nilimshangaa mama kwani hakushtuka hata kidogo tofauti na siku zingine, na gafla umeme ukakatika hapo ndipo uoga ulipozidi na kuendelea kumuamsha mama ambaye aliamka na kuongea kama mlevi kisha kulala tena.
Katika hali ile ya uoga nikapitiwa na usingizi palepale.
Yule mkaka wa ndotoni alikuwa anacheka sasa tena akicheka sana sana, kisha akaniambia nimpe mkono wangu nikasita kumpa na kukataa kabisa, akaniambia.
"Nakupenda Sabrina"
Nikamuangalia tu, akawa analazimisha kuwa nimwambie nampenda nikagoma akawa anataka kunichukua kwa nguvu.
Nikashtuka na kupiga kelele,
"Nampenda Sam"
Hapo mama nae akashtuka na kuniangalia kwa jicho kali sana.
"Yani wewe asubuhi Sam, mchana, jioni khee hadi ndotoni? Huyo Sam kakupa nini mwanangu?"
Akiuliza hayo, alikuwa akiangalia mwanga uliokuwemo chumbani na kugundua kuwa kumeshakucha teyari, akastaajabu sana kuona amepitiliza kulala kiasi kile.
Nikaenda kumuangalia na dada Penina ambaye nae alikuwa hoi na usingizi, nikamuamsha naye alishangaa kuona kumekucha kuasi kile.
"Mmh nimelala kama mlevi leo jamani"
Nadhani na wao hawakujielewa kama mimi niotaye ndoto za ajabu tu.
Siku ya leo kila mtu alikuwa na mawazo nyumbani kwetu, sijui na wao walipatwa na mandoto ya ajabu kama yangu. Nikawa nimetulia na kutafakari, ikaingia simu kuangalia mpigaji ni Lucy. Ile kupokea tu akanipachika swali,
"Sam unampenda humpendi?"
"Swali gani hilo la kuniuliza Lucy?"
"Kila swali ni swali na linahitaji majibu, jibu swali nililokuuliza.
"Unajua wazi jinsi gani nampenda Sam"
"Kama unampenda mbona unamsababishia majanga?"
"Majanga? Majanga gani?"
Lucy akakata simu, nikajaribu kumpigia Sam hakupatikana.
Nikampigia tena Lucy naye hakupatikana na kujikuta nikiwaza vitu vingi mno.
Nikafikiria sana na kukosa jibu, nikaamua kuvaa ili niende kwa Sam.
Kwavile ilikuwa ni jioni sana yani karibia na usiku, mama akanikatalia kutoka. Nikajikuta nikiwa na mawazo sana na roho kuniuma, muda wote nilimjaribisha hewani Sam alikuwa hapatikani wala Lucy nae hapatikani.
Siku hiyo nilikaa na dada kwenye luninga huku nikiwa na mawazo tu, ila badae dada alienda kulala na kuniacha mwenyewe pale sebleni. Saa sita usiku nikaamua kumtafuta tena Sam hewani na muda huu simu yake ikaita nikafurahi sana ili niweze kuongea naye na kupunguza mawazo yangu ila cha kushangaza hakupokea Sam bali ilipokelewa na Lucy.
"Sema shida yako haraka tunataka kupumzika bhana."
Niliiweka ile simu sikioni huku nikiwaza kuwa huyu ni Lucy kweli au yule jamaa wa kujigeuza. Mara nikashikwa bega na ile mikono ya baridi.
Itaendelea kesho......!!!!
Kama tuko pamoja
(y)
(y)
(y)
By, Atuganile Mwakalile.
HADITHI; Niliolewa na Jini bila ya kutarajia - 11
NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA 11:
Nilipogeuka ili kuondoka tu akanishika mkono na mkono wake ulikuwa wa baridi sana.
Ubaridi ule ulipenya kwenye mwili wangu hata nilihisi baridi na mimi, Carlos akaniangalia kwa makini kana kwamba anayasoma mawazo yangu.
"Mbona unaniogopa Sabrina? Mimi ni binadamu wa kawaida kama wengine jamani."
Nilibaki nikimuangalia tu, bila ya kumjibu kitu chochote.
"Kwani mimi nina pembe jamani? Au natisha? Kwanini uniogope Sabrina?"
Nikazidi kumuangalia na kuanza kumuuliza maswali na mimi.
"Kwani wewe ulijuaje kama simu yangu ilianguka?"
"Kwahiyo hicho ndio kinafanya uniogope?"
"Na je namba yangu uliitoa wapi?"
"Sikia Sabrina, siku niliyochukua simu ya Sam kuweka namba yangu ndio nikachukua namba yako humo. Halafu siku ile niliyokupigia nilijua tu umeshtushwa na simu yangu kwani nikasikia kama simu imeanguka na gafla ukapotea hewani ndipo nilipogundua kuwa simu yako imeanguka na kuharibika.
Roho ikaniuma sana kwani mimi ndiye niliyesababisha ndiomana nikaamua kwenda kukununulia simu nyingine kama ishara ya kuomba samahani. Tafadhari Sabrina pokea simu hii"
Ingawa nimeyaelewa maelezo ambayo Carlos ameyatoa ila bado iliniwia vigumu kupokea ile simu.
Mara mama akatoka ndani na kunikuta nimesimama na Carlos pale nje.
"Yani Sabrina muda wote umesimama na mgeni hapo nje? Kwanini usiingie nae ndani mwanangu! Haya karibu ndani baba.
Nikajua mama ameshapagawa na lile gari la Carlos pale nje, ikabidi nimkaribishe Carlos ndani ingawa sikuwa na imani nae.
Tukiwa tumekaa pale sebleni, mama akaanza kumuuliza maswali mawili matatu Carlos.
"Kwani wewe ni mwenyeji wa wapi baba?"
"Mimi ni mwenyeji wa mkoa wa Kigoma"
"Wazazi wako wako wapi?"
"Wazazi wapo Kigoma ila nina ndugu zangu baadhi hapa na wazazi nao watakuja tu maana wamekaa sana kule na wameshapachoka"
Carlos aliongea mambo mengi sana na mama, hadi kumwambia kuhusu simu aliyoniletea.
Mama nae akaanza kunilazimisha kuwa nichukue simu ile niliyoletewa na Carlos.
"Yani mama, mi sina nia mbaya kabisa kumletea Sabrina simu. Nimefanya hivi kama ishara ya urafiki wetu tu.
"Ndio namshangaa hapa kinachomfanya akatae, labda anahisi utamdai."
"Siwezi kumdai mama, nimemletea hii simu kwa hiyari yangu mwenyewe"
Mama akaendelea kunisisitiza kuwa niichukue, ikabidi niichukue ile simu na kumuuliza swali ambalo lilinitatiza bado.
"Mbona mikono yako ni ya baridi sana?"
"Hutokea tu ila si mara zote, nadhani nina upungufu wa madini flani mwilini"
Mama akaanza kucheka kisha Carlos akaaga na kuondoka.
Nilitafakari vitu vingi sana bila ya kupata jibu, kwakweli huyu Carlos alinifikirisha sana tena sana, hata nikashangaa kuwa mama amewezaje kumuamini Carlos kwa muda mfupi kiasi kile.
Mama akaja na kuanza kuniambia.
"Maskini jeuri wewe, simu unaitaka halafu unavunga! Kaka wa watu kajitokea mbali kwaajili yako eti wewe unavunga loh"
"Ila mimi simuamini yule kaka kabisa"
"Kwanini humuamini? Mbona ni mtu wa kawaida tu mwanangu!"
"Mi simuamini tu jamani"
Kwakweli sikumuamini kabisa Carlos niliona ni majanga tu.
Usiku ulipofika, mama alikuja kutembelewa na rafiki yake mama Salome.
Mama akaanza kumuelezea kuhusiana na matatizo yangu ya kuogopa ndani.
Nilikuwa kimya kwenye kochi nikijifanya nimesinzia ila nilisikia yote waliyozungumza.
"Sasa mama Penina, kama mtoto anawehuka hivyo wakati wa kulala kwanini msifanye maombi?"
"Hapo ndio hadi mi mwenyewe najishangaa mama Salome, yani Sabrina akianza kuwehuka huwa sikumbuki kabisa kusali hata sijui kwanini?
"Dunia imechafuka sana ndugu yangu, shetani ana jeshi lake kubwa humu duniani inatakiwa mkumbuke kusali kwani sala ni nguzo imara ya kumpinga shetani."
"Asante mama Salome nitafanyia kazi ulichosema"
"Tena kwa ushauri wa bure, ita familia yako tulia nayo mnaomba pamoja halafu mnalala"
"Nimekuelewa ndugu yangu.
Mama Salome akaaga na kuondoka kwani alikuja kumwambia mama habari za kikundi chao ila mazungumzo haya mengine yaliingilia kati tu.
Dada akarudi nyumbani, kwakweli leo alichelewa sana kurudi na alitukuta tunakula ilibidi mama amuulize sababu ya kuchelewa.
"Kuna mambo ya Fatuma namsaidia kushughulikia, nadhani kesho au keshokutwa tunaweza kufanikisha"
"Mambo gani hayo?"
"Nikiyasema sasa hivi kuna shoga yangu hapa atasema namtisha asilale, nitawaambia kesho kama nikirudi mchana"
Nikajua tu hayo mambo lazima yatakuwa yanahusiana na majini tu ndiomana hajayaongelea kwani anajua kuwa mimi naogopa sana mambo hayo.
Muda wa kulala ukafika, mama akainuka kwenda kulala na kuniacha na dada pale sebleni. Nikakumbuka maneno ya mama Salome kuwa tupende kusali kabla ya kulala, nikamfata mama na kumwambia kuwa amesahau maagizo aliyosema kwa mama Salome kuwa atayatelekeza.
Nikamkumbusha mama kusali naye akakumbuka, akarudi sebleni na kumwambia dada Penina kuwa tunatakiwa kusali kabla ya kulala.
"Mama, kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe, maswala ya kulazimishana kusali mimi hata siyapendi"
Dada Penina akawa anapinga kabisa ikabidi mama amuombe na kumlazimisha kuwa ni vyema tukifanya ibada ya pamoja, badae akakubali.
Kama familia tukaamua kufanya ibada kabla ya kulala.
Wakati wa ibada hiyo hakuna aliyeelewa nini kiliendelea kwani kila mmoja alijikuta yupo chumbani kwake asubuhi, na mama ndiye aliyekuwa wa kwanza kuja chumbani kwangu.
"Hivi muda ule tuliosema tunafanya ibada ilikuwaje?"
"Hata sielewi mama, maana sina kumbukumbu za ibada hiyo."
"Mmh ya leo kali!"
Dada Penina nae aliamka na kuja chumbani kwangu.
"Leo nimechelewa hadi kwenda kazini sijui hata ni usingizi wa aina gani!"
"Kila mmoja anashangaa hapa maana mara ya mwisho tulipanga kufanya ibada"
"Au tulifanya ibada na kwenda kulala?"
"Labda ila hakuna mwenye kumbukumbu yoyote."
Mimi nilikuwa natafakari tu na nikatambua kuwa yote yanafanywa na yule mkaka wa ndotoni tu kwani tuo afanyaye mambo ya ajabu.
Mchana nikampigia simu Sam, ambaye alikuwa na mawazo ya kupotelewa na pesa ya ofisi.
"Yani nimechanganyikiwa Sabrina, hata sijui pesa ya ofini nitaipatia wapi tena jamani mmh!"
Nikajaribu kumpa moyo na kumwambia maneno mazuri ambayo najua hayakumfariji hata kidogo kwani alikuwa ameshachanganyikiwa.
Nikapigiwa simu na rafiki yangu Suzy ambaye alianza tena kuniuliza kuhusu Carlos.
"Sabrina, unamuonaje Carlos?"
"Namuona ni mtu wa kawaida tu, kwani wewe unamuonaje?"
"Ngoja kwanza, nikimaliza uchunguzi wangu nitakwambia"
Suzy akakata simu, nikajiuliza maswali kuwa kwanini Suzy ana wasiwasi juu ya Carlos.
Mama akaniita na kuniambia kuwa ameongea na kaka na amesema kwamba hivi karibuni atanihitaji kwake ili nikabadilishe mazingira kidogo, kwakweli nilifurahi sana, hata dada aliporudi aliona jinsi nilivyofurahi.
Wakati wa kula dada akaamua kunitani,
"Naona umefurahi kuepukana na stori zangu za kutisha."
Mama akadakia,
"Lazima afurahi, anavyoogopa majini na watu waliofufuka huyu balaa"
Yani wanavyosema watu waliofufuka mie mwenzao ndio nazidi kupatwa na uoga wa mawazo.
"Anaogomba mazombie mdogo wangu jamani, ila mama yanatisha kweli yale usiombe ukutane nao
"Majini yako je hayatishi?"
"Mama wee usiniambie habari za majini, kilichompata Fatuma ni balaa"
"Mmeshaanza stori zenu sasa, mi mnanikera sana"
Ikabidi wanyamaze na tuendelee kula kama kawaida.
Usiku mawazo yangu yalikuwa ni kwenda kwa kaka tu, sikuwa na mawazo mengine zaidi ya hayo na sikutaka kukaribisha mawazo ya zaidi.
Wakati wa kulala ulipofika, nilikwenda chumbani na kulala moja kwa moja hata simu sikuongea nayo usiku.
Nikamuona Sam akihangaika sana, mara nikamuona akifunga ndoa na Lucy halafu tena nikamuona akitokwa na majipu mwili mzima. Nikashtuka kutoka kwenye ile ndoto na kujikuta nikianza kuogopa mule nyumbani, kwani wakati nimeshtuka nilikuwa nahisi kama mtu akitembea tembea mara avute kiti mara avute meza halafu sauti ikasika.
"Mbona umeamka kabla ya wakati Sabrina?"
Uoga ukanijaa, nikakumbuka maneno ya mama Salome kuwa natakiwa kusali.
Nikashuka kitandani na kupiga magoti, kabla sijafanya chochote taa ya chumbani ikazimwa halafu mikono ya baridi ikawa inagusa miguu yangu.
Kwakweli nilitetemeka kiasi cha kupoteza fahamu, sikupenda kutazama mbele na mara taa zikawashwa tena hapo nilizidi kutetemeka na hakuna maombi tena niliyoweza kuyafanya.
Nilijikunyata ukutani bila ya kujua cha kufanya, ile sauti ikajirudia tena.
"Mbona umeamka mapema Sabrina"
Kwakweli huu usiku ningeweza kuubadilisha basi ningeubadilisha jamani, jasho jingi lilinitoka na wakati nilikuwa natetemeka kwa baridi la uoga.
"Usiogope Sabrina, nipo nje ya chumba chako bado sijaingia ndani ila karibia nitaingia"
Mara gafla nikaona mlango wa chumba changu ukifunguliwa, muda huohuo mkojo ulinitoka bila ya hodi.
Itaendelea kesho......!!!
Kama tuko pamoja
(y)
(y)
(y)
By, Atuganile Mwakalile.







