
WASHINGTON, Marekani.
NDOA ya Rais Barak Obama na mkewe Michelle haitaweza kuvunjika kwa sasa kwa vile mke huyo mrembo atatakiwa kuendelea kuishi katika Ikulu ya White House hadi mumewe atakapomaliza muhula wake wa pili wa uongozi mwaka 2016.


Akifurahia jambo wakati mkewe kanuna.
Juzi, Gazeti la The Nation la Marekani liliripoti kuparaganyika kwa ndoa hiyo iliyowahi kutajwa kama ndiyo bora zaidi duniani, kwa kile kilichoelezwa kuwa kuchukia kwa Michelle baada ya kumwona mumewe akishoboka na Waziri Mkuu wa Denmark, Helle Thorning-Schmidt wakati wa shughuli za kumuaga rais wa zamani wa Afrika Kusini, hayati Nelson Mandela ‘Madiba’.

Helle akimuonyesha kitu Obama. Mwaka 2012, uvumi ulisambaa kwa kasi duniani ukielezea kutengana kwa watu hao wawili maarufu zaidi, hali iliyosababisha Ikulu ya Marekani kukanusha taarifa hizo.
Hata hivyo, hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, hakuna taarifa yoyote iliyotolewa na ikulu, Obama wala Michelle juu ya madai ya kutengana kwao.
Chanzo:- Vituko vya Mtaa
No comments:
Post a Comment