Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Stendi Kuu ya Zamani mjini Tabora, baada ya kumaliza ziara yake ya siku 11 katika mkoa huo, ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi
Wakazi wa Mji wa Tabora Mjini wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara uliondaliwa na CCM leo jioni,ambapo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana amehitimisha siku za ziara yake ya siku 11 mkoani humo,ya ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.Kinana na msafara wake kwesho wataelekea mkoani Singida kwa ziara siku kadhaaa tena.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara wa CCM, Mjini Tabora leo, ambapo aliwafananisha Wapinzani na Boko Haramu wa waasi wa Nigeria kwa kuwachonganisha wananchi kwa maneno,hali ambayo imeeleza kuwa kinaweza kusababisha vurugu nchini.
Katibu Mkuu wa CC,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM,Wilaya ya Tabora mjini mapema leo kabla ya kwenda kwenye mkutano wa hadhara,aidha Kinana katka ziara yake wilayani Tabora alikagua miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa umwagiliaji,kuweka jiwe la msingi katika ofisi za CCM,kukagua mradii wa ujenzi wa hospitali,kuzindua mradi wa matofali wa akina mama na mengineyo mengi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa na Wazee waasisi wa chama cha TANU mjini Tabora leo.
Kinana akinawishwa na Mamalishe kabla ya kupakuliwa msosi wa nguvu.
Kinana akihudumiwa na Mama Lishe alipokwenda kula yeye na msafara wake kwa akina mama lishe eneo la Stendi Mpya Tabora mjini. Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora, Munde Tambwe,kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Tabora, Aden Rage ukiungana na Kinana kula msosi kwa mamaLishe mjini Tabora leo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa wakipata mlo kwa Mama Lishe mjini Tabora leo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiapata mlo wa mchana kwa Mama ntilie katika stendi mpya ya mabasi mjini Tabora,Kushoto ni Mbunge wa jimbo la Tabora Mjini ,Mh Aden Rage,katikati ni Mbunge wa viti maalum CCM mkoani Tabora,Mh.Munde Tambwe wakishiriki pamoja na naye katika mlo huo sambamba na vijana wa mjini Tabora.
Naibu Waziri wa Maji,Mh.Amoss Makala akitoa ufafanuzi kwa wakazi wa Tabora mjini kuhusiana na suala zima la upatikanaji maji na mikakayi yake katika mkoa huo,ambapo imeelezwa kuwa mkoa huo una tatizo kubwa la maji
Baadhi ya Wabunge mbalimbali walioshiriki kwenye mkutano huo wa Hadhara uliofanyika mjini Tabora,ikiwa ni siku ya mwisho ya kuhitimisha ziara ya siku 11 ya katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mkoani humo.
Mbunge wa jimbo la Mtera,Mh.Livingstone Lusinde akiwahutubia wakazi wa mji wa Tabora mjini leo jioni kwenye mkutano wa hadhara uliondaliwa na chama cha CCM.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais,Mh. Ummy Mwalim akihutubia katika mkutano wa hadhara na kuuponda Ukawa kwa kitendo chake cha kutoka bungeni kwa sababu zisizoeleweka wakati wa Bunge la Katiba,Mh.Ummy pia aliwatia shime akina mama kuwa na mshikamano katika suala zima la kujiletea maendeleo katika nyanja mbalimbali walizomo,na kuacha kubweteka wakisubiri waletewe maendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa akihutubia katika mkutano wa hadhara wa CCM, ambapo alimpongeza Katibu Mkuu Kinana kwa kufanikisha ziara yake mkoani humo na kumaliza salama.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano ya Umma), Steven Wassira akihutubia katika mkutano wa hadhara na kuwaponda viongozi wa Ukawa wa kususia mkutano wa Bunge la Katiba bila kuwa na sababu za msingi.
No comments:
Post a Comment